Ugonjwa huu wa homa ya Denguo umeripotiwa kuathiri wilaya zote tatu (Kinondoni, Ilala, na Temeke) jiji Dar. Hadi wakati huu imeripotiwa wagonjwa 100 wameshapata maambukizi ya ugonjwa huu.

Mamlaka zimetoa tahadhari kwa wananchi kuchukua hatua za haraka kuzuia maambukizi ya ugonjwa huwo unaosababishwa na mbu ajulikanae kitalamu kwa jina la 'aedes egyptiae'

Kutokana na taarifa za kitaalamu zilizotolewa ni kwamba ugonjwa huwo wa homa ya Denguo unaweza kutibiwa kwa Panadol kushusha homa. Lakini mgonjwa haitakiwi kupewa Diclofenac au Asprin ambazo zinaelezwa kusababisha kutokwa na damu kwa wingi.



 
Top