Moto makali ukiwaka Eneo la Tukio Mbagala
Kwa Ufupi:
Wakazi 20 wa Dar wafariki dunia katika ajali ya Moto. Walikuwa katika
harakati za kuiba mafuta katika lori lililopinduka.
Hali ilivyokuwa ikionekana usiku wakati Moto ulipokuwa ukiwaka.
Eneo la tukio lililoungua Vibaya Usiku.
Habari Kamili:
Dar Es Salaam: Watu zaidi ya 20 mwanahofiwa kufa katika ajali ya moto uliotokea Mbagala Rangi tatu jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Chanzo cha moto huwo ni Lori la mafuta lililokuwa limepinduka katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tuki hilo walieleza kuwa Lori hilo lilidondoka wakati lilipokuwa likijaribu kukwepa gari nyingine ndogo iliyokuwa ikiingia barabarani pasipo kuangalia. Katika harakati za kulikwepa gari hiyo ndipo Lori hilo la mafuta lilipopinduka.
Baada ya tukio hilo, walifika wananchi wakiwa na vigaloni na mifuko ya Plastiki na kuanza kuchota mafuta kutoka kwenye tanki la gari lililokuwa limepata ajali.
Moto mkubwa ulizuka ghafla baada ya mtu mmojaaliyekuwa akijaribu kuchomoa betri alisababisha kutoka kwa cheche.
Moto huwo uliozuka uliunguza nyumba za kuishi, maduka pamoja na nyumba za kulala wageni. Vilele kwa habari zisizo rasmi inasemekana kuwa watu waliokuwa wamejuruhiwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili na Temeke.
Hadi sasa bado haijafahamika thamani ya mali zilizoteketea katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
UTAMU WA RAHA Inaendelea kufuatilia tukio hili kwa undani zaidi na itakufahamisha kilichojili na kinachoendelea.