Mwili wa Marehemu Ukiwa bado eneo la Tukio
Mtu mmoja mkoani Kigoma aliyefahamika kwa jina la Yusuph mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa kwenye korongo la Lubengera lililokuwa jirani na ofisi za CCM Mkoa.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii Kimeeleza kuwa Inasadikiwa kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Oktoba 13 kwasababu siku ya jana hadi jioni hapakuonekana mwili huwo.
Mili wa Yusuph umekutwa ukiwa na jeraha kubwa kwenye paji lake la uso, huku ikiwa haifahamiki chanzo cha kifo hicho.
Askari polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuelekea nao Central Police kwaajili ya Utaratibu mwingine.
Jhudi za kuutoa mwili wa Marehemu kutoka kwenye Korongo zikiendelea.
INNALILAHI WAINNA ILAIHI RAJIUN - BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE