Shekh Nasib Ali kama ambavyo cheo chake kinavyomtambulisha, amemwagiwa tindikali alipouwa anaoga kwa maandalizi ya kwenda msikitini.


SONGEA: Bwana Ally mkazi wa kijiji cha Kitanda wilayani Nantumboamemwagiwa maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali na alipokuwa bafuni anaoga majira ya saa 10 za Alfajiri alipokuwa akijiandaa kwaajili ya Ibada ya Alfajiri.

Watu hao waliommwagia tindikali Shekh walitoweka muda huohuo na kumuacha akilia kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyapata.

Ndugu na ma jirani walijitokeza na kumsaidia Shekh huyo na kumoeleka hospitali ya Pilamiho kisha baadae akahamishiwa hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu zaidi.




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Mskhiela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Juzi saa 10 Alfajiri. Pia akaeleza kuwa hadi sasa hakuna mtu ambaye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma hizo, hivyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi.



 
Top