Picha hizi zinaonyesha Midomo ya watu wenye maambukizi ya Magonjwa ya Ngono
Fanya haya yafuatayo mara tu unapobaini kuwa unamaambukizi ya magonjwa ya Ngono:
- Wahi kwenye kituo cha huduma ya afya kilicho karibu nawe kwa uchunguzi na matibabu sahihi.
- Tumia dawa zote kwa kufuata maelezo ya mtaalamu wa Afya hata kama dalili za ugonjwa zimepotea.
- Epuka kujinunulia dawa bila maelezo ya mtaalamu wa Afya.
- Usifanye tendo la ngono mpaka utibiwe na kupona kabisa.
- Muarifu mwenzi wako mapema ili wote mkapate matibabu sahihi na ushauri nasaha.
KUMBUKA:
- Athari za magonjwa ya ngozo zinaweza kuepukika ikiwa magonjwa ya ngono yatatibiwa mapema na kwa usahihi. Usiogope magonjwa ya Ngono yanatibika.
- Kuwepo kwa magonjwa ya ngono kunaongeza uwezekano wa kuambukizwa Virusi vya UKIMWI
- Kuwa mwangalifu wakati wote ili usiweze kuambukizwa magonjwa ya ngono, ikibidi kujamiiana tumia kondomu kwa usahihi.