Kufuatia Kuibuka kwa Mtandao wa Kitapeli Unaoitwa Tanzania Loan Society ambao unamhusianisha ndugu Ridhiwani Kikwete kuwa anaumiliki. Mheshimiwa huyo ameamua kuvunja ukimya na kuzungumza ukweli na wananchi kuhusiana na Mtandao huo.
Ameandika kwenye mtandao wa Facebook Kama ifuatavyo:
Habari zenu, mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale
wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma
habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .
Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza
kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu
yatanyooka.hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe. lakini
tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kukaba, kuiba au
kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au kikundi
fulani cha watu.
Hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata tweets juu ya kitu
kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine
kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Raisi Barack Obama
kuja Tanzania kupitia Raisi Dr. Jakaya Kikwete na sasa mie nikishirikiana na
Waziri Mkuu Bwana Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha.Jambo ambalo si la ukweli
hata kidogo na naomba tumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa
watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia
ninavyotuma kwenye kurasa hii.
Kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA
KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi
atakuwa AMETAPELIWA.
Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa
makini sana na mambo haya ya mitandao. maana wanaotangaza vitu kama hivi
wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU,
lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI
SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.
Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa muliamini
kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa
za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA
HAVIONJEKI
Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa
wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa maneno
pia. pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine wameathiriwa na
zoezi hili. lakini haukuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli
kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike na
kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza fanya jambo kumbe ndiyo unalikuza.
lakini pia niwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za face
book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli waone jinsi gani wanaweza
kulizungumzia jambo hili ili kuwasaidia wengi ambao wameathirika na imani yao
juu ya hili.
MIMI NDUGU YENU
JAKAYA MRISHO KIKWETE
AHSANTENI KWA KUSOMA TAARIFA HII