Mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyekuwa akisoma shule ya msingi Ananasifu ameshindwa kufanya mtihani wa kuhitimu Darasa la Saba kutokana na kufanyiwa unyama wa Kubakwa na kufungiwa ndani wakati wenzake wakiendelea na mtihani.
Dar Es Salaam: Bwana Thobias Gaspa Dibogo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Ostabay Jijini Dar Kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa miaka 14 na kumfungia ndani wakati wa kufanya mtihani.
Mama Mzazi wa Mtoto huyo, Elizabeth Macha amesema kuwa walipokea taarifa kutoka shuleni kuwa mtoto wao hakufika kwenye chumba cha mtihani siku hiyo kumalizia mitihani yake ambayo alikuwa amekwishaanza siku iliyopita.
Bi. Elizabeth aliendelea kusema kuwa walipofanya uchunguzi na kumfuatilia mtoto huyo walifanikiwa kumkuta Maeneo ya Kinyerezi kwenye nyumba ambayo alikuwa amefungiwa baada ya kubakwa.
"Kwakweli imetuuma sana tena sana kwa mtoto wetu kufanyiwa unyama kama huu. Tunaomba serikali itusaidie kwa hili" alisema James Tarimo baba wa mtoto huyo.
"Ninaomba nisaidiwe niweze kufanya mtihani wangu, ninaumia sana kwasababu maisha yangu ndio yameshaharibika" alizungumza huku akilia mtoto aliyefanyiwa unyama huyo.
Bwana Dibogo ambaye anatuhumiwa kufanya unyama huwo kwa kitoto hicho bado hakijaweza kung'amua baya na zuri, anashikiliwa na jeshi la pilisi ili kujibu mashtaka.