Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David A Msime
Watu wasiofahamika wamevamia Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM na kuandika maneno yenye Vitisho kwenye kuta za jengo hilo.
Dodoma: Katika hali ya kushangaza jengo la Makao makuu ya CCM mjini Dodoma limeonekana limepambwa ama kuchafuliwa na maandishi makubwa mekundu ambayo yamebeba ujumbe wa vitisho kwa wajumbe wanaohudhuria Bunge la Katiba.
Maandishi hayo yaliyokutwa asubuhi ya leo hii yalikuwa yakisomeka hivi "BUNGE LA KATIBA NI USFISADI"
Vilevile kulikutwa vipeperushi vimeenea sehemu mbalimbali za eneo hilo ambavyo vilikuwa vimebeba ujumbe wa vitisho kwa wabunge wanaohudhuria bunge la Katiba.
Vipeperushi hivyo vilisomeka kamaifuatavyo:
ONYO
Kesho hakuna mtu kuhudhuria Bunge la katiba, na Mbunge yeyote atakayekaidi na kufika bungeni atakiona chamoto"
Utamu Wa Raha Ilipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo.
"Hawa watakuwa ni wahuni tu ambao wanajaribu kuharibu amani ya nchi, Hakuna lolote ambalo litatokea ni vitisho tu" alizungumza mtu mmoja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa dodoma Kamishna msaidizi Muandamizi wa Polisi, David A Msime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Sehemu ambayo imetumika kuchapa Vipeperushi hivyo tayari imekwisha kufahamika. Hivyo wanafuatilia ili kuwapata watu waliohusika na tukio hilo ili kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria.