Sehemu za binadamu mwenye maambukizi ya Magonjw ya Ngono
Kuna aina mbalimbali za magonjwa ya ngono ambayo yamegawanya katika makundi kulingana na dalili zake kama ifuatavyo:
1. Magonjwa yenye dalili za kutokwa na majimaji au usaha sehemu za siri (Ukeni na uumeni), magonjwa hayo ni Kisonono, Trikomonas na kandida.
Uume wenye maambukizi ya Kisonono
2. Magonjwa yenye dalili za kutokwa na vidonda ambayo ni pamoja na Kaswende, Pangusa na Malengelenge sehemu za siri.
Uke wa mtu mwenye maambukizi ya Pangusa
3. Magonjwa yenye dalili za kutokwa na uvimbe ambayo ni Mitoki, Pangusa na Malengelenge sehemu za siri.
Kitu kimoja cha msingingi ambacho inabidi kieleweke ni kwamba, Mtu anaweza kuwa na maambukizi ya zaidi ya ugonjwa mmoja wa Ngono kwa wakati mmoja.
Kujitokeza kwa dalili za ugonjwa wa ngoni hutegemea aina ya ugonjwa wenyewe, jinsi na kinga ya mwili. Hata hivyo kuna baadhi ya watu huwa hawaoneshi dalili yoyote.
Asilimia 10 - 15 ya wanaume, na asilimia 60 - 70 ya wanawake wenye kisonono hawaonyeshi dalili yoyote. Hivyo basi, ni muhimu Kijana unapoelezwa na mwenzi wako uliyefanya naye tendo la kujamiiana kwamba ameambukizwa ugonjwa wa ngono usisite kituo cha huduma ya Afya kwa uchunguzi na tiba hata kama huna dalili.