Mwanamke mmoja amemfanyia ukatili mume wake kwa kummwagia maji ya moto yaliyokuwa yakichemka jikoni.
Mara: Mtu mmoma Mkoani Mara wilayani Bunda Bw. Malakila amelazwa katika hospitali ya DDH wilayani humo Baada ya kumwagiwa maji ya moto na mtu anayesadikiwa kuwa ni mke wake.
Chanzo chetu kimefika katika Hospitali ya wilaya ya Bunda DDH ambako Bwana Malakila amelazwa kwaajili ya matibabu.
Malakila ameelezea chanzo cha kufanyiwa unyama huo ni kuchelewa kurudi nyumbani kwa mke wake. Alisema kuwa mke wake alirejea majira ya saa nne za usiku kutoka sehemu ambako hapakufahamika.
"Nilipomuuliza kwanini umechelewa kurudi nyumbani aliniambia heti nimeanza makelele yangu, aliingia ndani na kuendelea kujibizana na mimi. Nilipatwa na hasira na kumfuata huko ndani na kutaka kumpiga lakini kulikuwa na bwana mwingine akanisihi nisifanye hivyo" alieleza bwana Malakila na kuendelea.
"Pale tulipokuwa kulikuwa na sufuria la maji ya moto jikoni, hivyo mke wangu aliinyanyua na kunimwagia nayo" alimaliza.
"Hapa duniani kuna binadamu wana roho za kinyama, yani mwanamke huyu ni mnyama mwenye ngozi ya binadamu. Tunaomba Serikali imchukulie hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wanawake wengine" alisema mwanamke mmoja aliyefika hospitalini hapo.
Mganga wa zamu wa hospitalini hapo Dr. Ibrahimu amesema kuwa bwana Malakila amepata matibabu na anaendelea vizuri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna msaidizi Philip Kalangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa mtuhumiwa ameshatiwa nguvuni, na atafikishwa mahakamani kwaajili ya kujibu shitaka.
Hospitali ya Bunda Designated District Hospita (DDH) alimolazwa bwana Malakila baada ya kuchomwa kwa maji ya moto.