Ajali hiyo iliyotokea saa 1.00 asubuhi jana, ilihusisha basi aina ya Coaster lililokuwa linakwenda Lushoto kugongana na lori hilo la Scania ambalo lilikuwa linakwenda Tanga mjini.


Muheza. Watu 11 wamekufa papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika Kijiji cha Mkanyageni, wilayani Muheza, Mkoa wa Tanga.

Ajali hiyo iliyotokea saa 1.00 asubuhi jana, ilihusisha basi aina ya Coaster lililokuwa linakwenda Lushoto kugongana na lori hilo la Scania ambalo lilikuwa linakwenda Tanga mjini.

Dereva wa basi dogo la Coaster, Bakari Mussa alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori aliyekuwa katika mwendokasi kushindwa kulidhibiti gari lake lililohama upande wake na kwenda kulivaa basi hilo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Peter Mwankai alisema miili ya marehemu hao 11 imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Muheza na tayari maiti saba zimekwisha tambuliwa na ndugu zao.

Alizitaja maiti zilizotambuliwa kuwa ni ya Moodi Muhamed, Zawadi Juma, Sister Christina, Ahmed Shemdoe, Asumani Masanja, Adam Shomari na Saumu Hassan. Alisema maiti tatu bado hawajatambuliwa.

Dk Mwankai alisema majeruhi 22 wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo na hali zao zinaendelea vizuri.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Ambrose Benedicto, Heri Frenimo, Ramadhani Kawote, Mwanaisha Hamdani, Hidaya Mohamed, Hassan Juma, Allan Charles, Paulo Moshi, Saleh Ali, Clara Lupari na Mwanaisha Rajabu.

Wengine waliojeruhi katika ajali hiyo ni Abubakari Salimu, Richard Kitala, Mwajuma Kasongo, Bahati Hussein, Mtaita Shangwe, Benjamin Abedi (dereva wa roli), Ramadhani Othman, John Fumeena na Ali Ibrahim.

Chanzo: Mwananchi
 
Top