Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya; ACP Barakael N. Masaki,
Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Henry Ambakisye (60) mkazi wa kijiji cha Kandete amekutwa ameuawa kisha mwili wake kutupwa mtoni.


Mwili wa marehemu Ambakisye umekutwa na jeraha lililotokana na kupigwa na kitu kizito utosini, katika mto huo mnamo tarehe 17/11/2014 majira ya 11: 00 asubuhi katika kijiji cha Kandete kata ya Kajunjumele wilayai Kyela mkoa wa Mbeye.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa, mnamo tarehe 15.11.2014 majira ya saa 23:00 Ambakisye alikuwa ameongozana na mwanamke Kisa Kima (48) mkazi wa Kapwili, alivamiwa na watu wawili na kuanza kumshambulia. Aidha mwanamke Kisa alipoona hali hiyo alichomoka na kukimbia eneo la tukio.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya; ACP Barakael N. Masaki, Amethibitisha kutokea kwa tukio hili na kusema kuwa mwanamke Kisa anashikiliwa na jeshi la Polisi kwaajili ya kuisaidia, halkadhalka watu waliohusika katika unyama huo wanatafutwa na polisi.

 
Top