BONGO DASLAAM Sehemu ya 6
Ilipoishia....
“Aaah!...No!...usitoe mkono. Naomba nikune pananiwasha” alisihi Suzy. Ayubu
ilimbidi afanye kile alichoagizwa na Suzy. Wakati Ayubu akimkuna Suzy alianza
kutoa sauti na miguno ya mahaba.
“Aaah!.... yeah!.....Oooh!..hapo hapo….Sweety….Mmm….tamu” alilalamika Suzy kwa
sauti ya chumbani huku akijilegeza na kujikuta akitaka kumlalalia Ayubu.
Endelea….
Sauti
ile ilifanya mapigo ya moyo wa Ayubu yaende kasi. Shetani wa mahaba alikuwa anamkaribia
kumkumba lakini alipokumbuka kuwa alichokuwa akitaka kukifanya ni kosa hasa kwa
wazazi wa Suzy ilimbidi ajikaze.
“Vipi Suzy?” Ayubu alihoji kwa sauti kavu
“A’m so sweety” Suzy alijibu kwa sauti ya mahaba iliyopenya kwenye masikio ya
Ayubu na kupita hadi moyoni. Alitamani kumkumbatia lakini akakumbuka tena kuwa
alikuwa anataka kumkosea mama Suzy. Alitoa mkono wake kwenye mgongo wa Suzy na
kutaka kusimama kuondoka lakini ilimuwia ngumu kutokana na askari kanzu
kusimama wima na bunduki yake mkononi. Alichofanya ni kusogea pembeni mbali
kidogo na pale alipokuwa amekaa Suzy.
“Mbona unaondoka Mpenzi”
“Mnh!” Ayubu alijifanya hakusikia swali aliloulizwa. Neno mpenzi ndilo lililo
mchanganya zaidi. Hakuwahi kulisikia kutoka mdomoni mwa mrembo yule pamoja na
vituko vyote alivyokuwa akimfanyia tangu alipoingia mle ndani. Hata hivyo Ayubu
bado hakuwa tayari kutembea na Suzy kwasababu alitambulishwa kama dada yake,
pia limhofia mzee Manyama kwasababu alimfahamu jinsi mzee yule alivyokuwa mtata
hasa kwa mtu aliyejaribu kucheza na binti yake. Ayubu alipokumbuka hayo mzuka
wote ulimuisha, aliinuka na kutoka nje akimuacha Suzy akiwa pekeyake sebleni.
Usiku Ayubu akiwa amelala chumbani kwake kutokana na uchovu wa mihangaiko ya
mchana alisikia malango wake ukigongwa. Aligundua kuwa aliyekuwa akigonga
mlango hakuwa mwingine zaidi ya Dada yake Suzy. Mwanzo alijifanya amelala
lakini kwasababu mgongaji hakuchoka ilimbidi kuinuka na kwenda kufungua mlango.
Lahaula! Alimkuta Suzy amesimama mlangoni kwake akiwa ndani ya nguo ya kulalia
iliyo onesha maungo yake ya ndani.
“Vipi dada Suzy kuna tatizo?”
“Ndio” alisema Suzy huku akiwa ameng’ata kidole na kuinamia chini
“Tatizo gani?”
“Naogopa kulala pekeyangu”
“Hee! Una…una….”
“Naogopa kulala peke yangu chumbani”
“Kwahiyo unatakaje”
“Sijui” alijibu Suzy kwa mkato.
“Suzy dadaangu, unaogopa nini wakati mimi nipo?”
“Mi siendi kulala huko, labda tulale wote huku kwako” Suzy alisema huku
akiminya minya vidole vyake vya mikono.
“Hapana dada Suzy, huwezi kulala chumbani kwangu wakati vyumba vipo vi…..”
“Hembu nipishe huko” kabla Ayubu hajamalizia sentensi yake, Suzy alimkatisha
kwa kumsukuma na kuingia chumbani. Alipofika alijitupa kitandani na kulala kama
mgonjwa aliyekuwa akisubiria uparesheni. Ayubu alihema kwa nguvu baada ya
kuuona mwili wa binti mrembo aliyeumbwa kila idara akaumbika. Ile nguo ya
kulalia ilipanda juu na kuacha mapaja yake wazi.
Ayubu alibaki mlangoni akijishauri cha kufanya. Alitamani kwenda kulala sebleni
lakini akawaza endapo baba yao angerejea usiku ule na kumkuta Suzy amelala
chumbani mwake ingekuwaje. Aliingia ndani kujaribu kumbembeleza labda
angekubali kwenda kulala chumbani kwake.
“Suzy dada, unajua sio kitu kizuri unachokifanya?” Ayubu alihoji kwa upole
lakini Suzy alijifanya hasikii. Alimgusa mgongoni na kumuita lakini bado
alinyamaza kimya.
“Naomba dada Suzy ukalale chumbani kwako” Alibembeleza Ayubu. Suzy alijikohoza
kisha akazungumza
“Kwanini hutaki nilale hapa?”
“Sio kitu kizuri”
“Mimi ni nani yako?”
“Wewe ni dada yangu”
“Sasa kwanini unaogopa kulala na mimi wakati ni dada yako?”
“Mmm!..aaah!...”
“Nini? kama mimi ni dada yako unahofia nini?”
“Basi wewe lala hapo mimi nitalala chini” alisema Ayubu baada ya kushindwa
kumshawishi mrembo yule kwenda kulala chumbani kwake.
“Vyovyote. Ukipenda hata kwenye kabati we lala tu” alijibu Suzy huku
akijipapasa kwenye mapaja yake mwenyewe.
Ayubu alichukua godoro lililokuwa juu ya
kabati na kulitandika chini kisha akatoka na kuelekea sebleni. Mambo aliyokuwa
akifanyiwa na Suzy yalikuwa yamekwisha mchosha. Alitamani wazazi wa Suzy
wangerejea hata usiku ule ili vituko vile angalau vipungue.
Alikaa kwenye kochi na kuwasha runinga.
Haikuwa lengo lake kutazama runinga usiku ule lakini ilimbidi kufanya vile ili
kumuepuka Suzy.
Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumamosi, Ayubu
alijikuta amelala palepale sebleni. Alikwenda chumbani kwa lengo la kumuamsha
Suzy akalale chumbani kwake, lakini alikutana naye mlangoni. Suzy alimtazama
Ayubu kwa jicho la hasira kiasi cha kumfanya Ayubu kupatwa na woga.
“Habari za asubuhi dada Suzy”
“Mbaya” Suzy alijibu kwa mkato
Ngugu msomaji Wetu wa simulizi hii ya kusisimua, Tupo tayari kukutumia kila toleo jipya la muendelezo wake. kitu cha kufanya LIKE Ukurasa wetu wa Facebook. BOFYA HAPA>>