
Ally aliongeza kuwa, tunasikia mtuhumiwa amesema marehemu ni jambazi ndiyo maana amempiga risasi, kitu ambacho siyo kweli hana historia hiyo na ni mgeni hapa jijini.
Akizungumza na gazeti hili Mtawala Amani ambaye nyumbani kwake ndiyo kulikuwa na mkesha wa harusi, alisema muda wa saa tatu aliamua kujipumzisha barazani aliamshwa mnamo saa tano na nusu na kelele zilizokuwa zinatokea nje ya nyumba yake.
Alisema baada ya kutoka nje alikuta damu na mwili wa kijana Muhasi na kuambiwa kuwa jirani yao Lucas Muhabi ndiyo amemuua kwa kumpiga risasi na muda siyo mrefu polisi walifika na kuuchukua mwili kuupeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mke wa Amani Pili Miraji alisema kuwa anamfahamu marehemu kwakuwa alikuwa akimuona anapita maeneo hayo kwenda kwa mjombawake ambako sio mbali kutoka hapo kwao.
Crdt: Mwananchi