Hilo linatokana na pointi ilizo nazo Chelsea kileleni ambazo haziwezi
kukaribiwa na klabu nyinginezo, ikiwamo Man United, ambayo baada ya kuanza
msimu vibaya imekuwa ikifanya vyema katika mechi zake za karibuni, kama
itaishinda Stoke.
London, England. Ligi Kuu England inaendelea leo kwa mechi kadhaa ingawa
haiwezi kubadili msimamo wa ligi hiyo, hasa kwenye nafasi za juu.
Hilo linatokana na pointi ilizo nazo Chelsea kileleni ambazo haziwezi
kukaribiwa na klabu nyinginezo, ikiwamo Man United, ambayo baada ya kuanza
msimu vibaya imekuwa ikifanya vyema katika mechi zake za karibuni, kama
itaishinda Stoke.
Baada ya kuilaza Hull City kwa mabao 3-0, Jumamosi, Man United inapigana
kikumbo kuzikaribia Man City na Southampton ambazo hazichezi hadi kesho, dhidi
ya Sunderland na Arsenal.
Mchezo mwingine unaosubiriwa kwa hamu ni baina ya Leicester na Liverpool.