
Mwili wa dada huyo baada ya kupigwa risasi na majambazi.
Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wanatumia
usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda, wamemuua kwa kumpiga risasi dada
mmoja ambaye jina lake halijafahamika.
Tukio hilo limetokea maeneo ya Kinondoni, Morocco jijini Dar
es Salaam baada ya majambazi hayo kuiba katika duka la M-pesa, wakati
wanaondoka walikuwa wanarusha risasi ovyo na kumpata dada huyu aliyekuwa
akipita njia.
Chanzo: Global Publisher