
Marehemu
waliotambulika kwa majina ni wanne ambao ni 1. Thomas Simfukwe (35) 2.
Exavery Mumbisa (34) 3. Amina Maiko (30) 4. Neema Almasi 5. Hebeli
Mkilimi 6. Rose Hezron Halele na 7. aliyefahamika kwa jina
moja Januari.
Watu tisa [09] kati
yao wanaume saba [07] na wanawake wawili [02] wamefariki dunia baada ya gari
waliokuwa wakisafiria lenye namba za usajili T.203 ARZ aina ya Toyota Coaster
lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye John Emanuel (36) mkazi wa
mlowo-mbozi likiwa linatokea Mbeya kwenda Tunduma wakati akijaribu kulipita
gari T.789 AZL/T.123 AXY aina ya Tata Truck eneo ambalo kuna mlima na mbele
yake kuna kona lilitokea gari T.903 CVF aina ya Tata basi hivyo dereva wa
coaster kulazimika kuingia mbele ya
lori alilokuwa analipita na kugongwa
ubavuni upande wa kushoto pia kugongwa upande wa kulia na basi aina ya Tata
tajwa hapo juu.
Tukio hilo limetokea
mnamo tarehe 21.12.2014 majira ya saa 14:10 mchana huko katika kijiji cha Chengula, kata na tarafa ya Tunduma, wilaya ya Momba, mkoa wa Mbeya, barabara
kuu ya Mbeya/Tunduma.
Marehemu waliotambulika kwa majina ni wanne ambao ni 1. Thomas Simfukwe (35) 2. Exavery Mumbisa (34) 3. Amina Maiko (30) 4. Neema Almasi 5. Hebeli Mkilimi 6. Rose Hezron Halele na 7. aliyefahamika kwa jina
moja Januari.
Hata hivyo miili ya
marehemu watatu bado kutambuliwa. Aidha katika ajali hiyo watu kumi na moja
[11] walijeruhiwa ambao majeruhi sita [06] wanaume, wanne [04] wanawake, wawili
wamelazwa katika hospitali ya rufaa Mbeya ambao ni dereva aitwaye John Emmanuel Mzumba (36) mkazi wa Mlowo na kondakta aitwaye Christian Mtende (31) mkazi wa Mlowo na wengine saba walipelekwa katika hospitali ya serikali wilaya ya Mbozi
na kituo cha afya Tunduma kwa matibabu.
Chanzo cha ajali ni
uzembe wa dereva wa toyota coaster kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake
bila kuchukua tahadhari.
Kamanda wa polisi
mkoa wa mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Ahmed z. Msangi anatoa
wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na
kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali
zinazoepukika.

Hii ndio coaster
iliyotoa roho za ndugu zetu maeneo ya sogea mlima chengula tunduma