Marehemu Neema
Malimbwi enzi za uhai wake.
WAKATI Wakristo kote nchini
wakijiandaa kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, keshokutwa Alhamisi, baadhi ya
familia zipo kwenye majonzi mazito kufuatia kuondokewa na ndugu zao, Uwazi lina
kisa cha kuumiza.
Jijini Dar es Salaam, binti mbichi
aliyejulikana kwa jina la Neema Malimbwi (pichani) ambaye alikuwa mwanafunzi wa
Chuo cha Kodi Tanzania (ITA) ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), kilichopo Mikocheni jijini Dar amefariki dunia kwa madai ya kulishwa
sumu kwenye kinywaji.
Marehemu Neema alikuwa binti wa
profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (Sua), Rogers Malimbwi.
SIKU YA TUKIO
Tukio hilo la kusikitisha linatajwa
kutokea usiku wa Alhamisi, Desemba 18, mwaka huu wakati Neema anarudi hosteli
maeneo ya Kijitonyama, Dar ambapo alikuwa akiishi.
ALIKWENDA KUJIRUSHA B BAND
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku ya
tukio, Neema alikuwa na marafiki zake wavulana kwa wasichana kwenye onesho la
muziki wa B Band inayomilikiwa na Banana Zorro ambapo akiwa huko saa 7 usiku
aliendelea kuchati na marafiki zake waliokuwa hosteli akitumia ukurasa wake wa
Facebook akiwaambia kuwa alikuwa ‘kiwanja’ akiponda raha.

Baba wa
marehemu Neema Malimbwi, Prof. Rogers Malimbwi.
Habari zinadai
kuwa, marehemu Neema usiku huo alikuwa akihama maeneo mbalimbali akiwa na
vijana ambao baadhi ya marafiki zake wanadai huenda walihusika na kumtilia sumu
kwenye bia alizokuwa akinywa.
MATATIZO
YALIPOANZA
Habari zaidi
zinasema kuwa, Neema akiwa na wenzake wakirudi hosteli, njiani alianza
kulalamikia kutojisikia vizuri.
“Alikuwa njiani
na wenzake wakirudi kulala, akaanza kulalamika kwamba hajisikii sawasawa,
ikabidi wenzake wamkimbize Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni,
Palestina, Sinza, Dar ambako waliambiwa kuwa kutokana na hali yake kuwa mbaya
wampeleke kwanza Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar ili
kupata hati ya matibabu (PF3),” kilisema chanzo kimoja.Chanzo hicho kikaendelea
kudai kwamba, walipofika Mabatini waliambiwa waende Kituo cha Polisi Oysterbay.
AKIMBIZWA
HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Ikazidi kudaiwa
kuwa, Polisi Oysterbay walitoa msaada kwa haraka ambapo sasa ikabidi Neema
akimbizwe Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala ambako
alifariki dunia.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius
Wambura (aliyesimama) akizungumza jambo.
ALIJITABIRIA KIFO
Chanzo hicho kilisema kuwa, denti huyo alikuwa kama
anafahamu siku ya kifo chake ambapo siku moja kabla alimshukuru Mungu kupitia
ukurasa wake wa Facebook kwa yote aliyomfanyia kisha kutuma picha mbalimbali
akiwa katika pozi tofauti.
MWILI WAKE MOCHWARI
Mwili wa Neema ulihifadhiwa kwenye mochwari ya Mwananyamala
kabla ya kusafirishwa juzi kwenda Morogoro kwa mazishi yaliyofanyika jana.
KUMBUKUMBU MBAYA
Kumbukumbu zilizopo kwenye makabrasha ya gazeti hili
zinaonesha kuwa, Juni Mosi, mwaka jana, mama mzazi wa Neema, Elizabeth Malimbwi
alifariki dunia kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar na mwili wake kwenda
kuzikwa Morogoro.
Tangu kifo cha mama yake, baadhi ya madenti wenzake
wanasema, Neema amekuwa akiishi maisha ya mawazo sana na muda mwingi alikuwa
akiutumia kunywa pombe kiasi kwamba, darasani ilikuwa mara chache sana
kuhudhuria.
Neema Malimbwi enzi
za uhai wake akiwa hosteli.
RPC ATHIBITISHA KIFO
Akizungumza na gazeti
hili juzi, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura
alikiri kuwa na taarifa hizo.“Ni kweli taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo
ninazo, mpaka sasa jeshi la polisi linasubiri ripoti kamili ya uchunguzi wa
madaktari kuhusiana na kifo chake,” alisema Kamanda Wambura.
Chanzo: Global Publisher