Watu watano wamefikwa na mauti wakiwemo wanandugu watatu baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka. 

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa watu hao walikuwa wakimpeleka ndugu yao hospitali kwaajili ya kujifungua. Gari ambayo ilihusika katika ajali hiyo T252 DCB aina ya Toyota Noah iliyokuwa ikiendeshwa na Ramadhan Masapala (32). Gari hiyo ilikuwa ikitokea kwenye kituo cha afya cha Miono na kuelekea katika Hospitali ya wilaya Bagamoyo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Uirich Matel amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa, ajali hiyo imetokea tarehe 5 majira ya saa 6:30 mchana eneo la Fuyakosi tarafa ya Msata wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda Matel amewataja watu waliofikwa na mauti katika ajali hiyo ni pamoja na dereva wa gari hio Masapara, Mnamisima Semhoro ambao ni wakazi wa Miono.

Majeruhi ni mjamzito aliyekuwa akipelekwa hospitali, Shukuru Jaba, na muuguzi wa kituo cha afya cha Miono Mariamu Omary.
Chanzo: Habarileo

 
Top