Baada ya
kukatwa utumbo mara tatu na kushonwa ameanza kupata nafuu “Mungu atanisaidia
nitapona,” alisema.
MTU mmoja, Mugusuhi Nyarusahe (39) mkazi wa Kijiji
cha Kinyambwiga wilayani Bunda, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
(ICU), cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara baada ya kucharangwa visu na
wenzake tumboni, katika kile kilichodaiwa kuwa ni mzozo wa mgawo wa fedha
zilizotokana na mauzo ya ng’ombe, tukio lililotokea wiki iliyopita.
Akizungumza akiwa hospitalini, Mugusuhi alisema
ameanza kujitambua baada ya kuzirai tangu alipochomwa kisu na kwamba baada ya
kukatwa utumbo mara tatu na kushonwa ameanza kupata nafuu “Mungu atanisaidia
nitapona,” alisema.
Jeshi la polisi kupitia kwa msemaji wake Kamanda ASP
Alex Kalangi limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa hakuna mtu
aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>