Mgombea mwenza wa urais kwa tiketu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Juma Duni Haji amewataka wagombea ubunge katika majimbo ya Buyungu Na Kasulu Mjini
Mkoani Kigoma kuheshimu uamuzi w a viongozi wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi - UKAWA wa kuachiana majimbo ili kuepuka kugawana kura na hivyo
kutoa mwanya kwa Chama cha Mapinduzi kuendelea kushinda katika uchaguzi mkuu wa
tarehe 25 mwezi huu .
Katika
jimbo la Buyungu Wilayani Kakonko ambako mgombea mwenza wa Urais , JUMA
DUNI HAJI amefika kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kuziguzigu na
kujikuta akishindwa kumnadi mgombea ubunge wa chama cha NCCR Mageuzi,MAWAZO
ATHANAS METHUSELA baada ya wananchi kudai kuwa mgombea anayekubalika katika
jimbo hilo ni wa CHADEMA Mwalimu KAFUKU BULAGO .
Katika
jimbo la Kasulu Mjini nako hali si shwari baada ya wagombea watatu wa vyama
vinavyounda UKAWA kujitokeza kwa pamoja kuwania kinyang'anyiro cha ubunge
katika jimbo hilo ambalo lilikuwa linaongozwa na MOSES MACHALI wa NCCR Mageuzi
kabla ya kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo.
Licha
ya migogoro hiyo, mgombea mwenza huyo wa urais amefanya mkutano mwingine katika
uwanja wa taifa jimbo la Muhambwe,mjini Kibondo na kuahidi kuwa iwapo wananchi
watamchagua EDWARD LOWASSA kuingia ikulu, atahakikisha anaijenga kwa kiwango
cha lami barabara ya Nyakanazi hadi Kidahwe.
Chanzo ITV
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA=>