Mwanamama aitwaye Sofia Mussa (65) wa Kijiji cha Tulieni kilichopo
katika tarafa ya Nakapanya, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, amefarika
dunia katika tukio la kushambuliwa kwa mapanga.
Baadhi ya mashuhuda wa mwili wa marehemu wamesimulia kuwa kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa shambani kwake akiendelea na kazi ya kung'olea mpunga.
Diwani wa Kata ya Nakapanya, Kubodola Ambali, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi, majira ya saa 3:00 asubuhi baada ya mama huyo kuvamiwa na watu hao wasiojulikana wakati akiwa shambani kwake.
Akizungumzia tukio hilo, mume wa marehemu, Sheikh Athuman Mohamed, alisema siku ya tukio, marehemu alikwenda shambani akiwa peke yake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mombeji, amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi.
Alisema kufuatia tukio hilo, jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Alifa Haji (30) kwa ajili ya kumhoji na kwamba, ikibainika kuwa ni miongoni mwa washiriki wa tukio hilo atafikishwa mahakamani.

Chanzo: Nipashe