Kufuatia mvuwa kubwa
zilizonyesha nchini Srilanka mamia ya watu wanahofiwa wamefunikwa na
vifusi vya maporomoko ya ardhi nchini humo.
Vijiji kadhaa katika maeneo ya kati ya kisiwa hicho yameathirika ambapo maiti 19 zimefukuliwa hadi sasa.
Shirika
la Msalaba Mwekundu linahofia hata hivyo kwamba watu 400 waliangukiwa
na maporomoko ya ardhi katika eneo la karibu na mji wa Aranayaka.
Juhudi
za kuwaokoa manusura zinakabiliwa na pingamizi kutokana na kuendelea
kuporomoka majabali na maji yanayotiririka kwa kasi kubwa.
Eneo la milimani,kilomita 100 toka mji Mkuu Colombo ni mashuhuri kwa mavuno ya chai na mpira.
Watu wasiopungua 46 waliuawa kufuatia siku nne za mvuwa kubwa nchini Srilanka.
Kutokana na mvua hizo kubwa za kusi,watu wasiopungua 200,000 na nusu walilazimika kuzihama nyumba zao.
Wakati
huo huo matumaini ya kuwapata bado wakiwa hai kiasi ya watu 150
waliokwama chini ya matope na vifusi yalididimia jana kutokana na mvua
kubwa inayoendelea kunyesha kutatiza shughuli za uokozi katika wakati
ambapo idadi ya waliokufa kufuatia janga hilo ikifikia watu 41.
Mvua
iliyonyesha kwa siku kadhaa sasa imelazimisha zaidi ya watu 300,000
kuyahama makazi yao katika nchi hiyo ya Kusini mwa Bara la Asia.
Data zinaonesha kwamba maiti za watu 18 ziliopolewa kutoka kwenye eneo la maporomoko.
Idadi
hiyo inatajwa kwamba huenda ikaongezeka kwa kasi kutokana na maafisa
wanaoendelea kupambana na hali ngumu inayosababishwa na tope jingi
kukata tamaa ya kuwafikia watu 134 wanaoaminika kunasa chini ya kifusi
cha jengo moja.