Kutokana na tukio la kusikitisha lilotokea hivi karibuni mwezi
Mei 8, mwaka huu saa nne asubuhi, la mwanaume mmoja kumbaka mtoto wa kike ndani
ya msikiti wa Kawawa, Liwale huko Lindi. Mahakama ya wilaya hiyo imemhukumu
mtuhumiwa huyo kifungo cha miaka 30 jela
Mahakama ya Wilaya hiyo ya Liwale chini ya Hakimu Mfawidhi,
Eric Ruhumbiza, imemtia hatiani
mshtakiwa kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 11, chini ya vifungu
namba 130 na 131 vya sheria ya makosa ya Kujamiiana (Sospa) ya mwaka 1998.
Hakimu wa mahakama hiyo amesema kuwa, mahakama imetoa hukumu
hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa upande wa mlalamikaji
mahakamani hapo.
Shahidi namba tano ambaye ni mtoto aliyefanyiwa unyama huwo,
ameiridhisha mahakama hiyo kutokana na maelezo aliyoyatoa kuhusu maumbile na
viungo vya siri vya mtuhumiwa.
Mwendesha Mashata ameeleza kuwa, kabla mshtakiwa kufanya
tukio hilo, alimuingiza mtoto huyo msikitini, sehemu ambayo wanawake
wanaswalia, alimlaza chini na kumvua nguo huku akimfunika kwa kanga usoni.
Aliendelea kueleza kuwa mshtakiwa kabla ya kumbaka mtoto
huyo alimuwekea kitabu kitukufu cha Quran kichwani na kumwambia kuwa kwa aya
anayomsomea, akimweleza mtu kitu atakachomyanyia atageuka kipofu.
Jambo hilo lilifahamika baada ya mfanya biashara katika eneo
la shule iliyopo karibu na msikiti huwo, kutilia shaka nyendo za mwalimu huyo
wa dini kuingia kwenye msikiti upande wa wanawake na kutoka kila mara
kuchungulia nje.
__________________________________________________________________________________________________