Baada ya gonjwa la Denguo saqsa ni ‘Panya road’ kujipatia
umaarufu jijini Dara.
Kundi linalodaiwa kuwa na vijana wenye umri wa kati ya miaka
12 – 17 limezuka jijini Dar na kuzua hofu kwa wakazi wa jijini humo hasa maeneo
ya Buguruni,magomeni , na Ilala.
Kundi hilo la ‘Panya Road’ ambalo maskani yake ipo Kigogo
mbuyuni, wamekuwa wakitembea kwa makundi makundi wakiwa na siraha za jadi kama
vile ,marungu, mapanga, mawe, na visu.
Vijana hao wamekuwa wakipita sehemu
mbalimbali huku wakipora mali za watu pamoja na kumpiga mtu yoyote ambaye
wanakutana naye, kwa silaha zao hizo ama kumfanyia jambo lolote ambalo
litamnyanyasa.
Hofu hiyo imepelekea maduka mengi kufungwa kwa kuhifia
vijana hao ambao wametokea kutikisa jiji ndani ya muda mfupi.
Vijana hao walianzisha vurugu hizo baada ya kijana mwenzao
ambaye inasemekena na mmoja wa kundi hilo kuuawa na wananchi kwa tuhuma za wizi
wa pikipiki, wiki iliyopita. Walianzisha vurugu hizo siku ya mazishi ambapo
walikuwa wakiwaibia watu na kuwapiga, jambo ambalo lilifanya mazishi hayo kuwa
na tafrani.
Kufuatia vurugu zinazoletwa na kundi hilo, wananchi
wameilalamikia serikali, ambapo kamanda wa Mkoa wa kipolisi wa Kinodnoni,
Kamanda Charles Kenyela alitoa tahadhari kwa kundi hilo na kusema kuwa sasa
wapo tayari kulidhibiti kwa nguvu za dola.
Pamoja na kauli hiyo bado kundi hilo la Panya Road
linaendelea kufanya vitendo vyake vya kudhalilisha na kuhatarisha maisha ya
watu wa jijini Dar.
Tahadhari ambayo inatolewa ni kwamba watu wanatakiwa kuwa
makini na makundi hayo ambayo huundwa kwa vijana wengi, wanaotembea kwa pamoja.