Jeshi la polisi linawashikilia watu wanne wanaodaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani Geita, Alphonce Mawazo.
Kifo cha
marehemu Mawazo kimetokea jumamosi hii Novemba 14 majira ya saa sita mchana
baada ya kuvamiwa na kundi la watu na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi.
Akizungumza na
waandishi wa Habari Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli
Mwabulambo amesema chanzo cha tukio ni kwamba kulikuwa na mkutano wa ndani ya
chama cha chadema uliofanyika ukumbi wa ludete b ulikuwa unahusu mambo yao ya
uchaguzi na walipokuwa wanaendelea katika kikao chao kuna mtu ambaye anadaiwa
ni mfuasi wa chadema na kumnong’oneza Marehemu mawazo na baada ya hapo wajumbe
walipata mshutuko na kutoka nje na wakakutana na kundi la watu na mtafaruki
ulianzia hapo.
Ameongeza kuwa
tatizo hilo kutokea kunahusishwa pia na itikadi za kisiasa lakini bado jeshi la
Polisi linaendelea na uchunguzi wake.
Hata hivyo
Kamanda Mponjoli amesema hali ni nzuri
maeneo ya katoro hasa kata ya ludete ambapo uchaguzi wa diwani umefanyika.
Chanzo: Star TV