Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki jijini Dar es Salaam wamegoma kuingia kazini ili kushinikiza uongozi wa kiwanda hicho kutekeleza madai mbalimbali wanayodai ikiwemo kuongezewa mishahara.
Chanzo chetu kilifika katika kiwanda
hicho cha Urafiki cha Urafiki kilichopo eneo la Ubungo jijini na kukuta
wafanyakazi hao wakiwa wapo nje baadhi yao wakiimba nyimbo mbalimbali za kudai
haki zao na wengine kuomba rais Dakta John Pombe Magufuli kuingilia kati sakata
hilo kwani wengi wao wanafanya kazi ngumu kwenye mashine lakini wanaamubulia
mishahara kiduchu.
Baadhi ya wazee walionekana
kuwa miongoni mwa wafanyakazi hao wamesema uongozi wa kiwanda hicho wameshindwa
kutekeleza agizo la mahakama ya usuluhishi ambayo ilisema uongozi wa kiwanda
hicho pamoja na chama cha wafanyakazi wakae pamoja ili kupitia majina ya watu
wanaotakiwa kulipwa ili zoezi hilo ifanyike lakini mpaka sasa agizo hilo la
mahakama imeshindwa kutekelezwa.
Licha ya kiwanda hicho kuwa na
wafanyakazi wa raia wa China, kutokana na ubia uliopo kati ya Tanzania na China
lakini raia wa China wanadaiwa kukimbia huku mmoja akionekana dirishani juu ya
gorofa akipiga picha kwa kujificha, ambapo naibu meneja mkuu msaidizi na meneja
utawala Bwana Moses Swai, amekiri wafanyakazi hao kuwa namadai ya muhimu lakini
amesema wapo katika hatua za mwisho hivyo akawaomba kuendelea na kazi.
CHANZO: ITV