Wananchi wa jimbo la Lulindi wengi wakiwa vijana wamesusia uchaguzi wa mbunge baada ya kutoridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu uliomalizika Octobar 25 mwaka huu kwa madai mfumo wa siasa bado umeegemea chama kimoja na si vyama vingi.
Chanzo chetu kimetembelea baadhi ya vituo katika kata za Chiungtwa, Namalenga, na Lulindi na kukuta sehemu kubwa ya vituo havina watu lakini pia iliweza kupita muda wa dakika tatu mpaka tano anajitokeza mpiga kura mmojammoja kama anavyozungumza msimamizi Romanus Charles.

Wengi waliojitokeza katika uchaguzi huo ni wazee wenye umri mkubwa na wakina mama wenye umri wakati, hata hivyo wagombea pia walijitokeza kupiga kura na wakawa na ujumbe huu.


Jimbo la Lulindi linawapiga kura elfu 59 miasita 19 huku likiwa na vituo vya kupigia kura 199, kata kumi na nane, limelazimika kurudia uchaguzi baada ya jina la mgombea ubunge wa CUF kukosewa.
Chanzo ITV

 
Top