Mwanamke huyo aliandika kwenye Facebook kuwa alikuwa anaenda
kumtembelea rafiki yake kabla ya kuuawa
Polisi nchini Japan wanachunguza kisa cha kushangaza ambapo
maiti ya mwanamke aliyeuawa ilitumwa kutoka Osaka hadi Tokyo kwa njia ya posta.
Inaaminika mwanamke huyo, Rika Okada, alidungwa kisu na
mwili wake kuwekwa ndani ya sanduku ambayo ilitiwa kibandiko na karatasi
iliyosema kuwa sanduku hiyo ilikuwa imemeba mwanasesere.
Sanduku hiyo, iligunduliwa ikiwa katika sehemu ya kuhifadhi
vitu katika kituo cha posta.
Polisi wanasema kuwa sehemu ambako sanduku hiyo ilipatikana
imewekwa, ilikuwa imekodishwa kwa kutumia kadi ya benki ya mwanamke huyo.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alitoweka tangu mwishoni
mwa mwezi Machi, alipotuma ujumbe wa mwisho kwenye ukurasa wake wa Facebook
kwamba alikuwa anaenda kukutana na rafiki yake wa muda mrefu ambaye alikuwa
hajamuona kwa miaka mingi.