Katika mkasa huwo watu watatu wamefariki dunia akiemo mtoto mchanga, na wengine kujeruhiwa vibaya, Kisesema.
Basi moja la abiria (Hice) linalofanya safari zake kati ya
Kilele na Kasulu, limerushiwa kitu kinachoaminika kuwa ni bomu lilipokuwa
likitokea Kilele kwenda Kasulu mjini Alfajiri ya leo hii maeneo ya Kisesema.
Kamanda wa polisi wa wilaya ya Buhige (OCD) Samweli Utonga, amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa watu wasiojulikana wamerilushia basi
hilo kitu kinachodhania kuwa ni bomu la kurusha kwa mkono na kusababisha vifo
vya watu watatu akiwemo mtoto mchanga.
Kamanda Samwel Utonga ameeleza kuwa majeruhi walifikishwa
katika hosptali ya Muyama, lakini kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi
wamehamishiwa katika hospitali ya Kasulu kwa matibabu zaidi.