Miongoni mwa abiria ambao walifariki katika ajali hiyo ni watoto watano, wanawake 6 na wanaume 6 (Wakiwemo madereva wa magari yote mawili)
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora, ACP Antony Rutta akitoa maelezo ya ajali kwenye eneo
la tukio kwa waandishi wa habari.
Watu kumi na saba wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba T570 AAM kupata ajali na kupinduka.
Basi hilo lilikuwa likitoka Tabora kwenda Mbeya. Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.
Miongoni mwa abiria ambao walifariki katika ajali hiyo ni watoto watano, wanawake 6 na wanaume 6.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi - Amin
Kwa habari mbalimbali LIKE ukurasa wetu wa Facebook Hapa>>