Serikali imeombwa kupeleka haraka vifaa vitakavyoweza kusaidia kugundua wagonjwa wa ugonjwa wa Ebora Tunduma mpakani mwa Zambia na Tanzania.
Wananchi wa Tunduma wamesisitiza kuwepo na kifaa maalumu kitakachoweza kusaidia kugundua watu walioadhirika na ugonjwa huwo hasa kwa watu wanaopita kutoka nchini Zambia. Wananchi hao wamezungumza na Utamu wa Raha Leo na kueleza kuwa, pamoja na kwamba kumekuwepo wageni wengi wanaoingia kutoka Nchi za jirani lakini hakuna tahadhari yoyote ambayo imechukuliwa kuzuia ugonjwa huwo.
Hata hivyo Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na vyombo mbalimbali kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Ebora nchini Tanzania.