Kwa ufupi
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 14
jijini Dar, amelazwa hospitali ya Temeke huku akiwa na dalili zote za kuwa na
ugonjwa wa Ebora.
Kwa mujibu wa taarifa za mganga
mfawidhi wa hospitali ya Temeke Dr. Amani Malima amethibitisha kuwepo kwa msichana
huyo hospitalini hapo.
Msichana huyo ambaye aliingia nchini
jana akitokea Benin, Afrika Magharibi alionekana kuwa na dalili za ugonjwa
huwo. Kwani baada ya kuhojiwa na madaktari alisema kuwa anahisi maumivu makali
ya viungo, miguu na mikono alieleza Dr.Amani.
Mganga huyo ameendelea kutoa maelezo
yake kwa kusema kuwa baada ya kumfanyia vipimo msichana huyo alibainika kuwa na
malaria, lakini vipimo vya ebora bado havijatoa majibu ambapo majibu yake
yatatoka leo. Aliongeza kuwa endapo msichana huyo hata gundulika na maambukizi
ya ugonjwa huwo watamruhusu.