![Photo: Kama kweli una macho mazuri heb niambie hizo ziko ngapi....? dah! ila bado naikumbuka tunzo yangu moja iloibiwaga zamani...watu bwana, eti naskia waliambiwa na mganga ili mimi nishuke waniibie tunzo yangu moja halaf waipeleke kwake......
[if you really gat Strong eyes please tell me How many trophies
are there...? ]](https://scontent-b.xx.fbcdn.net/hphotos-xap1/t1.0-9/p280x280/10612704_783697801652036_6584403555507296400_n.jpg)
Kwa Ufupi:
Walioiba walitumwa na Mganga ili waweze kumfanyia mazingara Diamond kumshusha nyota yake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipa nchini Diamond Platnuz (Nasibu Abdul) ambaye ameibuka kidedea na kuibuka na tuzo za kutosha katika matamasha mbalimbali, Ameamua kuanika tuzo zake hadharani na kujivunia kazi ya akili yake. Kwa namna moja ama nyingine masanii huyo ambaye alistahili kupokea tuzo hizo anastaili kupewa pongezi na kuwa mfano wa kuigwa hasa katika kazi zake.
UTAMU WA RAHA imemnasa msanii huyo akiwa amezipanga tuzo zake na kuzitupia mtandaoni huku akijisifia na kuonesha kukumbuka moja ya tuzo yake iliyoibiwa kwa lengo la kufanyiwa mambo ya kishirikina, kama alivyodai mwenyewe.
"Kama kweli una macho mazuri heb niambie hizo
ziko ngapi....? dah! ila bado naikumbuka tunzo yangu moja iloibiwaga
zamani...watu bwana, eti naskia waliambiwa na mganga ili mimi nishuke
waniibie tunzo yangu moja halaf waipeleke kwake..... [if you really gat Strong eyes please tell me How many trophies are there...? ]" Aliandika Diamond katika mtandao fulani wa kijamii.