Moto ukiendelea kuteketeza Jengo la msikiti
Kwa Ufupi
Mdikiti wa Mtambani jijini Dar, unateketea kwa Moto ambao umeanza majira ya swala ya Magharibi hadi muda huu.


Habari zilizotufikia, Msikiti wa Mtambani unaungua, na moto huo umeanza wakati wa swala ya maghrib. Hadi sasa sehemu ya juu  ambayo ni ghorofa ya tatu imeshateketea yote, jitahada za wananchi na jeshi la uokozi na zimamoto wanaendelea kupambana kuuzima moto huo. Chanzo cha moto huo kinasadikiwa kuwa ni umeme japo hakuna uthibitisho rasmi kutoka jeshi la polisi ama jeshi la uokozi na zimamoto. Ghorofa hiyo ya tatu sehemu kubwa ni madarasa ya sekondari na ofisi za Walimu.                    Sehemu ya juu ya Ghorofa hili ni madarasa na ofisi za walimu

Wananchi pamoja na askari wa zima moto wanaendelea na jitihada za kuuzima Moto huwo ambao tayari umeshateketeza sehemu ya juu ya ghorofa hilo.

Hadi sasa bado chanzo cha moto huwo unaoendelea kuteketeza jengo la msikiti bado hakijafahamika ingawa tetesi zilizopo ni kuwamba umesababishwa na hitilafu ya umeme.

Kwa habari na Matukio zaidi Ungana na Ukurasa wetu wa Facebook hapa>>

 
Top