Staa wa Real Madrid, Di Maria ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2010
akitokea Benfica anahatihati ya kuuzwa na timu hiyo baada ya kugoma kusaini
mkataba mpya.
Mchezaji huyo Di Maria ambaye kwa wakati huu amekuwa
akihusishwa kuwa na mpango wa kujiunga na klabu ya Manchester United, katika
kipindi cha msimu huu anahofiwawa kuwa na wakati mgumu Santiago baada ya timu
hiyo kuchukua uamuzi wa kuwasajili James Rodriguez na Toni Kroos.
Kwa mujibu wa Kocha mkuu wa Real Madrid, Carlo Ancelotti,
amethibitisha kuwepo kwa suala hili na kueleza kuwa, hawana budi kumuuza Streka
huyo aliyechezea timu hiyo zaidi ya mechi 100 tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2010, kwasababu amegoma kusaini
mkataba mpya na ameomba kuhama.
Hata hivyo Ancelotti, ameeleza kuwa mchezaji huyo ataendlea kubaki
katika klabu hiyo endapo atakuwa amekosa pa kwenda.