SIMULIZI YA KUSISIMUA - Sehemu ya Pili
Walimzogoma na kumlazimisha alipe pesa ya watu vinginevyo wange
muitia kelele za mwizi apigwe hadi kupoteza uhai.
Pamoja na kwamba hakuwa na mtu aliyekuwa upande wake lakini
hakukata tamaa ya kujitetea. Hatimaye walifikia hitimisho la kuosha masufuria
ili kufidia gharama za chakula alichokula
bwana hapa hakuna mtu” walisema wale watu na kuondoka kwa
kukimbia. Ayubu alivuta pumzi na kuzitoa kwanguvu. Hakuamini kama ameweza
kuokoka kutoka mikononi mw. Baadaya ya kumaliza adhabu aliyopewa ilikuwa
imekwishafika jioni. Alitembea tembea huku akifikiria mahali ambapo angeweka
ubavu wake usiku huwo. Hadi inafika mida ya saa nne alikuwa hajatambua mahali
pa kulala.
Mungu hamtupi mja wake. Alipata kauchochoro na kujilaza. Kwakuwa hakuwa na nguo
ya kujifunika alihisi baridi ikimtesa sana. Alijikunja na kuwa kama kifaranga
aliyepoteza mama muda mfupi uliopita.
Ilipofika
usiku wa manane akiwa pale kwenye kiuchochoro alisikia sauti za watu
wakizungumza huku wakitembea kuelekea pale alipokuwa amelala. Aliwasikia
wakijibishana.
“Huyu jamaa anapenda kulala maeneo haya”
“Inabidi tuwe makini, huyu mtu ni hatari”
“Ni kweli”
“Tulieni, twendeni kimyakimya”
“Ok”
Walivyokaribia wakammulika kwa tochi na kumuona Ayubu amelala.
Ayubu alivyoona vile alishindwa kuvumilia akaanza kutimua mbio ili kuokoa
maisha yake. Wale watu nao walimuunganishia kwa nyuma na kumkimbiza huku
wakipiga firimbi kama vile walikuwa wakimkimbiza mwizi.
Ayubu alipofika mbele alikumbana na mtu ambaye naye alikuwa
akikimbia kuelekea kule alikokuwa akitokea yeye. Wote wawili walidondoka chini
kisha waliinuka na kutimua mbio kila mmoja alielekea upande wake. Ayubu
hakuamini kama amepona kutoka kwa yule mtu, kichwani mwake alifikiria kuwa yule
alikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wanamkimbiza.
Kundi kubwa la watu likatokea mbele yake huku wakipiga
makelele ya mwizi. Hapo Adamu akagundua kuwa kumbe yule mtu aliyekumbana naye
alikuwa ni mwizi. Uamuzi aliochukua ni kupinda kushoto kuwakwepa. Lo! Kumbe
walimuona na kuanza kumkimbiza yeye.
Kwakuwa alikuwa mgeni katika zile njia alizokuwa akipita,
alitumbukia kwenye mtaro wa maji machafu. Alitaka kuinuka na kuendelea kukimbia
lakini aliteleza na kuanguka tena. Wale watu walikuwa wamekwisha mfikia.
alijivuta hadi kwenye karavati lililokuwa karibu na kujibanza sawia na ukuta.
Wale watu walifika na kuuruka ule mtaro kwa spidi wakiamini kuwa
Ayubu alikuwa amepita. Mmoja kati ya wale watu akasikika akiwashauri wenzie
waangalie kwenye mtaro pengine mtu wao alikuwa ameingia humo.
Mwanga wa tochi ulimmulika Ayubu machoni na kumfanya kufumba macho
na kutulia akisubiri matokeo. Alibana pumzi ili asionekane. Akasikia sauti za
watu wakibishana.
“Oyaa twendeni bwanaa hawezi kuingia hapa”
“Kwanini asiingie, anaweza kuwa humu humu”
“Haya mulika na kule kwenye karavati”
“Twendeni a watu wale. Alipoona kuwa kumetulia na hapakuwepo na
dalili ya kuwepo na mtu maeneo yale, alitoka taratiibu kwa umakini wa hali ya
juu.
Wakati Ayubu akitoka alisikia sauti za watu wakielekea pale
alipokuwa yeye huku wakiongea. Ayubu alijirudisha na kujibanza kando ya
karavati. Wale watu walifika na kusimama juu ya lile karavati. Mara alihisi
vitu kama maji ya moto yakimdondokea usoni na kutiririka hadi usawa wa mdomo.
Lo! Kumbe mmoja kati ya wale watu alikuwa akikojoa. Harufu ya ule mkojo ilimfanya
Ayubu kubaini kuwa yule mtu alikuwa amekunywa pombe.
Kulipo pambazuka Ayubu alikuiwa amechoka sana na nguo zake
zilikuwa chafu mno. Alikuwa ananuka mwili mzima. Aliangaza huku na kule pengine
angepata maji ya kujiosha lakini hakuambulia kitu. Alianza kuzurula vile vile
ili kutafuta msaada wa mavazi lakini kila alipofika walimfukuza na
kumuita chizi.
Ilipofika mchana alihisi njaa ikimsumbua, mfukoni hakuwa na hata
shiringi moja. Alipokwenda kuomba watu wamsaidie alifukuzwa kutokana na kuwa
mchafu na kutoa harufu. Waswahili wanasema “Msafiri kafiri” Ayubu alikuta
chakula kimemwagwa jalalani. Kwa njaa aliyokuwa nayo alikifakamia chakula kile.
Watu waliomuona walishindwa kumtofautisha na vichaa walioko mjini. Baada ya
kumaliza chakula chake alianza kuzurula tena huku akilini mwake kukiwa na wazo
la kumtafuta rafiki yake Kondo.
Ilipofika jioni akajikuta akitamani kupata chakula cha usiku.
Mfukoni mwake kulisalia harufu ya matope tu. Alielekea kwenye jalala moja na
kupekua pekua. “Jasho la mtafutaji halimwagiki bure” alifanikiwa kupata mkate
na viazi vilivyopikwa. Alitia kwenye mfuko wa rambo na kuondoka nao. Safari
yake ilikuwa haifahamiki mwisho ingawa lengo la safari ile lilikuwa ni kumsaka
rafiki yake Kondo.
Alifika kwenye kiuchochoro alijibanza kwa lengo la kupata
chakula ambacho alikiokota
Kule
jalalani. Sehemu aliyokuwa amekaa ilikuwa imetulia vizuri. Haikuwa rahisi kwa
mtu yeyote kuweza kumuona kirahisi. Alifungua mfuko wake na kuanza kula
taratibu huku akifikiria mahali pa kulala usiku ule.
Sauti
za miguu zilisikika zikielekea pale alipokuwa ameketi. Mara akaona kivuli cha
watu wawili waliokuwa wakizidi kumsogelea. Ayubu alijisogeza nyuma taratiibu na
kujifunika na tenga lililokuwa pembeni yake. Watu wale walifika na kusimama
pembeni ya lile tenga.
Ayubu
alikuwa akiwaona vizuri kwa kupitia kwenye tundu. Walikuwa wameshikilia mapanga
yaliyokuwa yamelowana kwa damu. Ayubu aligundua wazi kuwa watu wale walikuwa
wametoka kufanya mauaji mahali fulani. Mtu mmoja miongoni mwao aliinua mguu na
kuupachika juu ya lile tenga. Ayubu alibana pumzi kuzuia mapigo ya moyo ambayo
yalikuwa yakimuenda kwa kasi.
“Vipi,
hapa panafaa?” mtu mmoja alihoji.
“Inaonekana
panafaa”
“Mnh!
Watu hawafiki hapa?”
“Hata
kama wakifika hawawezi kujua kama kuna mali”
“Enhee!
Umeona hilo tenga?”
“Lina
nini?”
“Tufiche
humo ndani”
“Hembu lifunue” sauti
ya mtu yule ilizidi kumshitua Ayubu na kumfanya atetemeke. Alifahamu wazi kuwa
watu wale waliokuwa na silaha zilizokuwa zimelowa damu, wasingeweza kumuacha
akiwa hai. Ayubu alifumba macho na kumuomba Mungu atende miujiza.
Endelea hapa>>
Endelea hapa>>