Wema Sepetu Msanii wa filamu
 Kajala Masanja Msanii wa Filamu

Waswahili wanakwambia 'Wapendanao ndio wagombanao na wagombanao ndio wapatanao' Kauli hii imejidhihirisha kwa wasanii wa tathnia ya filamu nchini, Wema Sepetu na Kajala Masanja.


Wasanii hawa wawili ni watu ambao walikuwa wakipendana sana na kushibana kuliko kawaida kiasi cha kufikia hatua ya Wema Kumlipia Faini Kajala ya shilingi milioni 13 ili kuzuia kufungwa kwa rafiki yake huyo kipenzi.

Ghafla mapenzi ya wawili hao yalisambaratika na kila mmoja akawa kivyake. Jambo hili lilizua maneno kwa mashabiki wao huku kila mmoja akizungumzia kivyake chanzo cha kutengana huko.

Mgogoro wao ulikuwa ukizidi kukua mkubwa kila kulipokucha na maneno tofauti tofauti yalienea kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari yakizungumzia chanzo cha bifu hilo.

Pamoja na yote ambayo yamezungumzwa kuhusiana na chanzo cha mgogoro huwo, ukweli ni kwamba chanzo cha mogoro ni kupishana kwa kauli kitu ambacho ni cha kawaida sana kwa kila binadamu.

Kitu kibaya zaidi ambacho kilichochea utofauti huwo ni kwenye mitandao ya kijamii ambako kumezuka makundi ya pande mbili ambayo yamekuwa yakichochea hali hiyo huku mashabiki hao wa pande hizo mbili tofauti wamekuwa wakirushiana maneno machafu yakiwemo matusi ya nguoni.

Hata hivyo wawili hao walipatana na kila mmoja akionekana kujutia hali ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo kwa kipindi kirefu.

“Mimi nilikuwa napenda sana kukuangalia wewe na siyo timu zinazotuzunguka zinazidi kututia chumvi tugombane, nakupenda na ninajua ni rafiki mwema kwangu lakini unasikiliza sana maneno ya watu,” ni maneno ya Kajala yaliyosikika akimwambia Wema.

“Najua hivyo na wewe unafahamu nakupenda sana na ni rafiki ninayefurahi tukiwa pamoja nikiwa nawe siku zote,” alijibu Wema.
 Wema na Kajala picha ya pamoja baada ya Kupatana

Baada ya wawili hao kupatana, mashabiki wa pande zao wakabakia wamejawa na aibu wasijue la kuzungumza na kupepesa macho yao kwa haya na aibu. Hata hivyo mashabiki hao wameonekana kuwa na nguvu za kuwazidi kiasi cha kuwafanya wawili wapendanao wahitirafiane tena na kuwa kama paka na chui.

Hali hii inaonesha kuwa kupatana tena kwa wasanii hawa ambao ni kioo cha jamii ni ndoto hasa kama wataendelea kuwasikiliza mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii ambao kila kukicha wamekuwa wakiandika maneno ya uchonganishi kwa wawili hawa.

Ujauzito wa Snura Kuyeyuka>>

 
Top