Msanii wa Mduara Snura akiwa katika pozi
Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa msanii wa
mduara Snura kuwa amepata ujauzito, hatimaye meneja wake, Mohamedi Kavu HK amesimama
na kuzungumzia suala hilo.
Huku ikiaminika kuwa msanii huyo amehamia kwa
mpenzi wake mkoani Mbeya,meneja Mohamedi Kavu amekanusha mbele ya mapapalazi taarifa
za msanii huyo kuwa na ujauzito.
“Hana mimba. Yupo Afrika Kusini, anashuti
video yake lakini tunatarajia baada ya wiki mbili atakuwa amerudi.” Alisema Kavu.
Meneja HK alipozungumza na mapaparazi alisema
kuwa Snura alikuwa akitarajiwa kuingia nchini Oktoba 10 mwaka huu.