Akizungumzia
utafiti huo mhadhiri wa Uhandisi wa Mazingira kutoka Chuo kikuu cha Ardhi ‘Aru’
Willium Mwagoha alisema waligundua mabwawa ya majitaka
yanayotoka mabibo, dampo la vingunguti, viwandani na gereji mbalimbali
yanamwaga maji kwenye mto huo.
Dk.Mwegoha
alisema mboga zilizomwagiwa maji hayo zilibainika kuwa na sumu zilizokuwa na
madini ya risasi,shaba na kromiamu ambazo zote zina madhara kwa binadamu.
Aliasema
katika utafiti huo walibaini kuwa mboga hizo zinauzwa kwenye masoko
ya Ilala, Kariakoo, Buguruni, Veterani,Tazara, Mwananyamala, Mnyamani,
Kigogo, Kisutu, Vingunguti, Tabata, Mikoroshini na maeneo ya jirani na wkaulima
hao.
Crdt: Nipashe