Wakazi wa jiji la Dar es salaam wapo katika hatari ya kupatwa na magonjwa makubwa kamasaratani, utasa, kupoteza uwezo wa kuona,kuharibu ubongo,maini na figo kutokana na matumizi ya mboga za majani zinazolimwa katika mabonde ya jiji hilo.


Matumizi ya mboga hizo ni makubwa jijini humo,yakitokana na umuhimu wake kwa afya  za watu na hali duni ya maisha inazozifanya familia nyingi kumudu gharama zake ikilinganishwa na vitoweo vingine.


Sehemu kubwa ya mboga hizo inatokana na kilimo kinachofanyika katika mbonde la mto Msimbazi namaeneo ya Kigogo-Sambusa,Ubungo,Gereji mchicha,Vingunguti na Tandale.


Katika Gazeti la NIPASHE limesema tayari matokeo ya tafiti kadhaa yamedhihirisha maji yanayotumika kwa umwagiliaji  wa mboga za majani jijini humo kuwa na kemikali zenye sumu ama taka zinazotoka viwandani na kwenye makazi ya watu.


Pili wakazi wanaoishi pembezoni mwa bonde la Msimbazi na maeneo mengine yanayolimwa mboga hizo,wamebainika kutupa taka kama betri zilizoisha muda wa matumizi,masalia ya simu za mkononi,vipuri vya magari na majokofu mabovu.


Taka hizo zenye sumu zinatupwa kwenye mifereji ya maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga hivyo kuzidi kuhatarisha afya za walaji.
 

Chuo Kikuu cha Ardhi kilifanya utafiti katika bonde la mto Msimbazi na udongo na maji kwa vigezo vya Shirika la Afya dunia WHO  na Shirika la viwango nchini TBS. Endelea>>

 
Top