Watu sita wamefariki na wengine Arobaini na tatu Kujeruhiwa mkoani Singida katika ajali mbili tofauti zilizo husisha basi la Nice Line kuligonga Lori kwa nyuma na Noah iliyokuwa ikienda kwenye msiba kupinduka.
Akithibitisha kutokea kwa vifoo
hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktali Daniel Tarimo,
amesema watu watano wamekufa katika ajali ya basi na moja amekufa katika ajali
ya gari dogo aina ya Noha na wamepokea majeruhi arobaini na tatu wakiwa
wamevunjika miguu na kulazimika wengine wanne kuondoa kabisa sehemu za miguu
ambayo ilikuwa imesagika na kushindikana kuungwa.
Wakielezea baadhi ya abiria,
majeruhi na mashuhuda wamesema dereva wa basi alikuwa katika mwendo wa kasi na
kwakuwa ilikuwa usiku hakuweza kuyaona magari mawili yaliyokuwa yame
haribika na alipoamua kukwepa gari moja alitoka nje ya barabara na kukanyaga
kingo za baraba na kusababisha kuyumba na kuligonga lori lililokuwa limeegeshwa
pembezoni mwa barabara likiwa bovu.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hizo
kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema ajali
zote mbili zimesababishwa na mwendo kasi pamoja na uzembe wa madereva kuto kuwa
makini barabarani na mimehusisha basi la Nice Line lenye usajili wa namba T 174
CAV Scania lilokuwa likitoke Dar-es-Salaam na kueelekea Mwanza kuligonga roli
namba RAT.317n/rl.o754 na ajali ya Noha yenye usali wa namba T.998 CWG iliyo
kuwa ikitokea Dar-es-Salaam na kuelekea Kahama kwenye msiba.
Chanzo: ITV