Jeshi tayari lipo katika eneo la tukio kwaajili ya kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia mamlaka husika.
Mamlaka ya
kukabiliana na majanga ya dharura NDMA imesema kuwa imepokea maagizo kutoka kwa
Nawaz Sharrif kuchukua hatua za dharura.
Jeshi tayari
limepelekwa katika eneo hilo kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili
kuisaidia mamlaka hiyo.
Wengi wa
waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.
Maafisa wa afya
wanasema vifo vingi vimetokea katika mji mkuu wa Karachi ambao ulikumbwa na
joto la viwango vya juu vya hadi digree 45 c.
Katibu wa afya
katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo amesema kuwa watu 612 walifariki katika
hospitali kuu ya serikali mji huo katika kipindi cha siku nne zilizopita.
Wengine 80 wameripotiwa
kufariki katika hospitali za kibinafsi.