Zoezi la uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam, lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam limekamilika na hivyo Isaya Mwita wa CHADEMA kuibuka mshindi kwa kupata kura 84, Omari Yenga CCM kura 67 na kura 7 zimeharibika,wajumbe walikuwa 158.
Kinyang’anyiro cha Umeya katika uchaguzi huo polisi waliimarisha ulinzi kila pande kwa lengo la kuhakikisha kuwa amani inakuwepo mahala hapo na zoezi hilo liende kama lilivyo pangwa.
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA VICENT MASHINJI na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA,Edward Lowassa pamoja na mbunge wa Arusha mjini Mh.Godbless Lema na makada wengine wa chadema ni miongoni mwa watu walioshiriki katika zoezi hilo lililofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi huo wa Meya wa Dar es Salaam umefanyika leo baada ya kuahirishwa mara kadhaa kwa sababu mbalimbali ikiwamo zuio la Mahakama ambalo lilitupiliwa mbali na mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kuamauru uchaguzi ufanyike leo