Akiwa amefungwa kamba baada ya kufumaniwa
Kijana
Saimon Dustan Mwanjavala ‘Mwachakala’ (15), mkazi wa Kijiji cha Mbwila Kata ya
Luana, Wilaya ya Ludewa mkoani hapa, amepoteza maisha kufuatia kupigwa na kaka
yake wa tumbo moja baada ya kumfumania katika zizi akila uroda na nguruwe.
Tukio hilo la aina yake lilijiri saa 8 mchana wa
Novemba 17, mwaka huu ambapo kaka mtu huyo alimkuta mdogo wake ndani ya zizi
hilo akiwa katikati ya starehe na nguruwe.
Habari
zinadai kuwa, baada ya kushuhudia kitendo hicho kaka huyo alimshika mdogo wake
na kumfunga kamba miguuni na mikono kwa nyuma kisha akaanza kumpiga kwa fimbo
mwilini.
Akiwa amevuliwa nguo zote baada ya kufumaniwa
Inaelezwa kuwa, wakati wa kipigo kutoka kwa kaka yake,
marehemu alikuwa akijitetea kwa kusema kwamba alilazimika kuingia kwenye banda
la nguruwe kwa ajili ya kuondoa hamu ya mapenzi kutokana na kubanwa zaidi bila
kupata mwanamke.
Licha ya utetezi huo, kaka mtu alimvua nguo zote mdogo
wake na kuendelea kumwadhibu mpaka akapoteza maisha.
“Baada ya kuona mdogo wake amepoteza maisha, kaka mtu
alilazimika kuuacha mwili chini, akachukua sumu ya panya na kutoweka
kusikojulikana,” alisema shuhuda mmoja.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Wilbroad Mtafungwa alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kuongeza kwamba hadi sasa jitihada za kumsaka mtuhumiwa
zinaendelea.
Kamanda Mtafungwa aliwataka wananchi kutokujichukulia
sheria mkononi kwani hata kama kijana huyo alikutwa akifanya mapenzi na nguruwe
bado hukumu yake haikuwa kifo.