ELIMU duni ya njia salama za uzazi kwa wajawazito, imekuwa kikwazo na kufanya vifo vya wajawazito na watoto kuendelea.
Meneja wa Shirika la World Lung Foundation mkoa wa Kigoma, Adolf
Kaindowa amesema vifo hivyo vinaendelea kuwepo, licha ya kuboreshwa kwa
vituo vya kutolea huduma na kujengwa kwa vyumba vya upasuaji katika
vituo mbalimbali mkoani Kigoma.
Alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahudumu wa afya katika jamii.
Mafunzo hayo yalihusu utoaji elimu na uhamasishaji jamii kutumia njia
salama za uzazi wa mpango. Yalilenga kupunguza vifo vya wajawazito na
watoto mkoani Kigoma.
Kaindowa alisema bado wajawazito wengi, wameendelea kujifungulia
nyumbani na kwa wakunga wa jadi, badala ya vituo rasmi vya utoaji
huduma, hivyo kuchelewa kupatiwa huduma, jambo linalochangia kufanya
vifo vya wajawazito na watoto kuendelea.
Alisema sababu kubwa ya kuendelea kwa hali hiyo ni jamii kutotambua
umuhimu wa wajawazito kuzalia vituo rasmi vya utoaji huduma na kukimbia
gharama za kununua vifaa vinavyotumika wakati wa kujifungua.
Mratibu wa Shirika la Engender- Healh mkoa wa Kigoma, Dk Wilfred
Mongo alisema bado akinamama wengi hawana uelewa na elimu sahihi ya njia
salama za uzazi wa mpango.
Chanzo: HabariLeo
HABARI NA MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>
Chanzo: HabariLeo
HABARI NA MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>