Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limefanikiwa kudhibiti wimbi la wanawake kubakwa na kujeruhiwa na vijana wanaojulikana kama Tereza baada ya kuendesha msako na kuwakamata vijana 30 wanaotuhumiwa kuunda genge linaloendesha vitendo hivyo mitaani nyakati za usiku.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi Ferdinand Mtui amesema watu hao ambao wamekamatwa katika maeneo
ya Vamia Mwanga na Katubuka watafikishwa mahakamani mara baada ya
upelelezi kukamilika na kwamba wamebaini kuwa maeneo yanakotokea matukio
hayo ya ubakaji hakuna umeme,nyumba nyingi hazina milango imara na
maeneo hayo yamezungukwa na vilabu vya pombe.
Kwa upande baadhi ya wakazi wa mjini Kigoma,wamesema uwepo matukio
hayo ya ubakaji umesababisha hofu katika jamii ambapo wamelitaka Jeshi
la Polisi kufanya uchunguzi zaidi wa suala hilo na kulipatia ufumbuzi wa
kudumu ili kuondoa hofu katika jamii.
Chanzo: ITV