Aliyeluwa bondia wa kwanza maarufu mweney asili ya Kiafrika,
Muhammud Ali, wa Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka
74.Kulingana na msemaji wa familia yake, bingwa huyo wa
zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote duniani kwa sababu ya
machachari yake katika ngumi, alifariki katika jiji la Phoenix Arizona,
baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.
15.00pm:Floyd Mayweather Jr:Leo moyo wangu
unanung'unika kwa kumpoteza mwanzilishi ,bondia hodari,bingwa na shujaa
kwa vyovyote vile.Hakuna siku niliingia katka ulingo wa ndondi bila
kukukumbuka ,alisema katika mtandao wa instagram.Ucheshi,uzuru wako na
vyenginevyo ndio vitu tutakavyovienzi.
14.00pm:George Foreman:Aliyekuwa mwanamasumbwi
George Foreman aliyewahi kupambana na Mohammed Ali katika mechi
iliofanyika Zaire kabla ya Ali kuibuka mshindi anasema kuwa Mohammed ali
alikuwa na ushawishi wa kukufanya akupende.Iwapo usingempenda
angekufanyia vituko zaidi ndio uweze kumchukia zaidi.
13.00pm:Muhammad Ali alijiunga na masumbwi kwa bahati.
Ali
aliyekuwa na umri wa miaka 12 alikuwa na marafikize waktafuta peremende
na porp corns za bure.Na alipogundua kwamba baiskeli yake imeibwa
aliagizwa kwende chini ya nyumba aliyokuwepo katika taasisi ya mafunzo
ya Columbia ambapo afisa wa polisi Joe Martin alikuwa akisimamia mpango
wa ndondi.Martin alimwelezea Ali kwamba angeanza kunoa ngumi zake kwa
kujifunza ndondi kabla ya kumtafuta mwizi huyo.Kwa haraka alijua vile
ambavyo angejichukulia na alipofika umri wa miaka 18 alikuwa ameshinda
dhahabu ya Olimpiki mjini Rome.
12.30pm:Wasifu wa Muhammud Ali12.00pm:Aliyekuwa bingwa wa ndondi katia uzani mkubwa duniani Muhammud Ali amefariki.
Aliyekuwa
bondia wa kwanza maarufu mweney asili ya Kiafrika, Muhammud Ali, wa
Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.Kulingana na
msemaji wa familia yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu,
anayejulikana sana kote duniani kwa sababu ya machachari yake katika
ngumi, alifariki katika jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa
hospitalini Alhamisi.Alikuwa na matatizo ya kupumua, hali ambayo
ilitatanishwa zaidi na maradhi ya Parkinson, ambayo ni hali ya mgonjwa
kutetemekatetemeaka.Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya
mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.Alipozaliwa alipewa
jina la Cassius Marcellus Clay.
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>