Habari zilizotua kwenye dawati la Wikienda
zinadai kuwa, jike dume huyo hufanya biashara katika nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki hususan jijini Kampala (Uganda), Bujumbura (Burundi),
Nairobi (Kenya) akitokea pia Dar es Salaam (Tanzania).
ANATUMIA JINA LA QUEEN
Kwa mujibu wa chanzo, Ivan baada ya
kujibadili na kuwa katika mwonekano wa mwanamke hujiita Queen kwa maana
ya jina la kike, wanaume wengi wanaomjua akiwa hivyo humwita kwa jina
hilo.
“Uzuri wake si rahisi kutambua kuwa ni
mwanamke kwani amekuwa akijipamba, anatumia manukato ya kike na
anapoingia kwenye klabu za usiku, hujichanganya na warembo wengine
waliotoka kwenda viwanja ili kutofahamika kuwa ni mwanaume,” kilisema
chanzo.
Akiwa anasoma kitabu nyumbani kwao.
SASA MKASA WAKE WA KUKAMATWA NI HUU
Mkasa mzima wa kukamatwa kwa jike dume
huyo hivi karibuni nchini Uganda ulianza pale alipokutana na mwanaume
mmoja ambaye hakujulikana jina mara mmoja.
Mwanaume huyo alitokewa na ‘Queen’,
akaingia mzimamzima na baada ya mazungumzo, aliamua kumlipa kabisa chake
na kumtaka waende kwenye nyumba ya wageni ‘gesti’ moja jijini Kampala
kwa ajili ya kumalizana kama makubaliano yao yalivyo.
AKATAA KWENDA NYUMBA YA WAGENI
Inadaiwa kuwa, baada ya malipo hayo
ambayo kiasi cha pesa hakijatajwa, Bebeto alikataa kwenda nyumba ya
wageni na kumtaka mteja wake huyo waende kwenye nyumba aliyodai kuwa,
huwa anahifadhia mizigo yake huku akimsisitizia kuwa atafurahi kwa
sababu watakuwa wote usiku mzima.
Akiwa katika pozi.
Ikazidi kudaiwa kuwa, kutokana na
mtazamo wake, mwanaume huyo alimshtukia Bebeto kwamba anaweza kuwa mtu
mbaya, ndipo aliamua kuwajulisha polisi wa kituo hicho ambao walifika
haraka sana kumkamata.
MAMBO HADHARANI
Baada ya tukio la kukamatwa, ndipo
aligundulika kuwa, Bebeto ni kidume na si mwanamke na hajawahi kuwa
mwanamke tangu azaliwe hali ambayo iliwashangaza na polisi wenyewe.
WATU KIBAO KITUONI
Habari za mwanaume kukamatwa kwa madai
ya kujibadili kuwa mwanamke ili apige pesa zilisambaa kwa kasi, watu wa
eneo hilo wakakusanyika kituoni Katwe kwa ajili ya kumshuhudia Bebeto na
kila aliyemuona hakuamini kutokana na uzuri aliokuwa nao lakini
alipovua wigi alionekana kichwa chake halisi ingawa hata kama asingekuwa
na wigi bado ilikuwa vigumu kumjua ni ‘meni’ mpaka kumchunguza.
AFUNGULIWA RB
Polisi wa Kituo cha Katwe waliamua
kumfungulia kesi kijana huyo yenye faili la kumbukumbu REF65/04/11/2016
ambapo ameshikiliwa mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni.
Chanzo: Ijumaa Wikienda