Takriban watu 20 wamefariki papo hapo baada ya basi moja la watalii kuanguka kutoka juu ya mwamba karibu na eneo la kujivinjari lililopo Kusini mwa Uturuki.
Watu wengine 11 walijeruhiwa wakati dereva alivyopoteza mwelekeo wa basi hilo dogo na kugonga kizuizi.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa hakuna watalii wa kigeni waliokuwemo katika basi hilo.
Takriban watu 400 walikuwa wameabiri basi hilo kulingana na gavana wa mkoa wa Mugla, Amric Cicek ambaye anasema huenda breki zilifeli.
Lakini Meya wa eneo la Marmaris ,Ali Acar aliambia gazeti la Uturuki la Hurriyet nadhani ajali hiyo ilisababishwa na makosa ya dereva.
Vyombo vyengine vya habari vinasema kuwa waathiriwa wengi walikuwa wanawake na watoto. 
Chanzo: BBC

Soma Mkasa Huu: Jambazi wa Kike auwawa na Polisi
 
Top